Alvina Gachugu AKA ‘Alvina.’ s story appeared in the Taifa leo Magazine
here down is the story
Kwa Mukhtasari
Huenda akadharauliwa na wengi kutokana na kimo chake, lakini ni msanii anayeendelea kuitikisa tasnia ya burudani kwa kibao ‘Mama’ ambacho kimemtambulisha kama msanii.
USIDHARAU wembamba wa reli, gari la moshi linapita; ndiyo msemo unaoweza kumtambulisha mwanadada Alvina Gachugu al-maarufu ‘Alvina.’
Huenda akadharauliwa na wengi kutokana na kimo chake, lakini ni msanii anayeendelea kuitikisa tasnia ya burudani kwa kibao ‘Mama’ ambacho kimemtambulisha kama msanii.
Tueleze kwa kifupi kuhusu maisha yako.
JIBU: Nilizaliwa miaka 22 iliyopita. Nilisomea katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, Nairobi, nilikomaliza Kidato cha Nne mnamo 2010.Baadaye nilijiunga na Shule ya Muziki ya Kamata nilikosomea masuala ya muziki. Kwa sasa ni mwanafunzi wa Uanahabari katika Chuo Kikuu cha St Pauls’, Nairobi.
Kibao chako ‘Mama’ kimepata umaarufu mkubwa nchini. Ni siri gani ambayo umetumia kujizolea
mafanikio hayo?
JIBU: Kwa kweli, ‘Mama’ ni mojawapo ya vibao vingi ambavyo nimetunga, ila kimeibukia kupata umaarufu mkubwa, hali ambayo imenifanya kutambulika na hata nyimbo zangu nyingine kufahamika na mashabiki. Safari yangu ya muziki imekuwa ndefu.
Ulianzaje?
JIBU: Kwanza, nilijitosa katika muziki katika hali ninayoweza kutaja kama kimakosa. Nilifanya majaribio yangu ya kwanza kuingia katika muziki nikiwa ningali katika shule ya upili, nilipojaribu kujiunga na kwaya ya shule, ila nikakatazwa mara mbili. Hilo halinikuvunja moyo. Nilipata nguvu na kubuni kikundi changu cha muziki kilichowashirikisha wanafunzi wenzangu. Hapo ndipo nilinoa kipawa changu, na kukipiga msasa zaidi nilipomaliza kidato cha nne.
also read Little Mix – Wings (Cover by Alvina Gachugu, Kenya … – YouTube
Baada ya kumaliza kidato cha nne?
JIBU: Nilishirikiana na mwanamuziki mmoja kutoka Tanzania aitwaye Kaka Radi, aliyenijumuisha kama mwanamuziki msaidizi katika albamu yake. Cha kushangaza ni kuwa nilishiriki katika nyimbo za taarab zikiwemo: ‘Chawa Kunguni’, ‘Jirani’, ‘Nisemeni’ na ‘Wema’. Ni baada ya hapo niliamua kufanya muziki peke yangu.
Ni nyimbo zipi zingine ulizoweza kurekodi?
JIBU: Kwanza, nina albamu ninayoshughulikia kwa sasa itakayoitwa ‘Bon Appetit’. Hili ni jina la Kihispania linalomaanisha ‘Furahia Upendo’. Nyimbo zingine zitakazokuwepo ni kama: ‘Comfort Zone’ (nilioshirikiana na mwanamuziki Vini Shema), ‘Mi Queribo’, ‘My Baby’, ‘Deepest Love’ kati ya vingine.
Mbona unaimba kwa Kihispania na Kifaransa ilhali mashabiki wengi nchini wanafahamu Kiswahili na Kiingereza?
JIBU: Lo! Ni uamuzi wa kimakusudi wa kuwavutia mashabiki wengi. Nyimbo zangu nyingi huwa za Kiswahili na Kiingereza. Vile vile, kando na mapenzi ninaangazia masuala mengine kama uhifadhi wa mazingira, uzalendo, elimu, nafasi ya mtoto wa kike kati ya mengine.
Kando na muziki, unafanya nini kingine?
JIBU: Ninajivunia kuwa na vipawa vingi, kwani huigiza pia. Nilianza kuigiza vitabu vya fasihi vya shule za upili pindi baada ya kukamilisha shule ya upili kati ya 2011 na 2012. Kutokana na umahiri wangu, nimeshiriki katika michezo mingi ya kubuni katika ukumbi wa Alliance Francaise na Kenya National Theatre (KNT). Pia nimekuwa nikiendesha hafla za kimuziki za Karaoke katika mkahawa kama Casablanca kati ya mingine.
Ushauri wako ni upi kwa wasanii wanaoibukia?
JIBU: Kutokufa moyo kwa lolote walifanyalo.